Mazungumzo ya “Frusa ya dunia katika kuimarisha mageuzi ya China katika zama mpya” yamefanyika tarehe 29 Julai mjini Nairobi, Kenya. Mazungumzo hayo yaliandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG). Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong alitoa hotuba kwa njia ya video. Naye Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhou Pingjian pia alishiriki kwenye mazungumzo hayo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi, mkuu wa taasisi ya utafiti wa sera za Afrika ya Kenya, na mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Kenya walitoa hotuba, na kufanya mazungumzo juu ya umuhimu wa Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, na fursa za Afrika zinazoletwa na China katika kuimarisha zaidi mageuzi kwa pande zote.
Bw. Shen Haixiong alipotoa hotuba alisema Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) siku zote linadhamiria kueleza vizuri habari za China juu ya mageuzi na kufungua mlango, na maendeleo ya kisasa yenye umaalumu wa China. Pia linajitahidi kuhimiza mawasiliano kati ya China na dunia. Anatumai wadau wote watahimiza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kupitia mazungumzo ya dhati.
Mkuu mtendaji wa Chuo Kikuu cha Nairobi Bw. Stephen Kiama alisema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” linaifanya Afrika ione uwezekano wa ushirikiano wa kunufaishana. Nchi za Afrika zinaweza kupata uzoefu kupitia mageuzi na ufunguaji mlango wa China pamoja na ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Mkuu wa taasisi ya utafiti ya Afrika juu ya mambo ya China Bw. Patrick Maluki alisema, katika miaka ya karibuni, China imepata matokeo mazuri katika mageuzi ya kiuchumi, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na ushirikiano wa kimataifa, na inaipatia Kenya ufumbuzi katika kukabiliana na changamoto kwenye sekta za teknolojia ya kidigitali na nishati isiyoleta uchafuzi.
Mkuu wa taasisi ya utafiti wa sera za Afrika ya Kenya Bw. Peter Kagwanja alisema baadhi za nchi za magharibi zinaweka vizuizi vya biashara, lakini China inatoa pendekezo la maendeleo ya dunia, pendekezo ambalo linatafuta njia mwafaka katika maendeleo ya siku za usoni.
Naibu mwenyekiti wa jumuiya ya Wakenya waliosoma China Bw. Joseph Maritim alitoa wito kwa nchi za Afrika kutumia vizuri fursa ya kuimarisha mageuzi nchini China katika zama mpya, na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China kwenye sekta mbalimbali ili kutimiza maendeleo ya pamoja.
Ofisa mkuu mtendaji wa Baraza la Wahariri la Kenya Bibi Rosalia Omungo alisema mageuzi ya China yanaleta fursa kwa vyombo vya habari vya nchi za kusini, na kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya Afrika na China kunaweza kujenga jukwaa lenye ufanisi zaidi na kuleta uwezekano zaidi katika kujenga dunia yenye pande nyingi chini ya msingi wa ustawi wa pamoja.
Mkuu wa idara ya lugha za Asia na Afrika iliyo chini ya CMG Bw. An Xiaoyu aliwaelezea wageni moyo na umuhimu wa Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China. Alisema duru mpya ya mageuzi ya China inatoa hatua zaidi ya 100, ikiwa ni pamoja na sekta za siasa, uchumi, utamaduni, jamii n.k. China inaendelea kuhimiza maendeleo yenye ubora na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuifanya dunia inufaike na fursa ya China na kutimiza kunufaishana.
Walioshiriki kwenye mazungumzo hayo waliona kuwa shughuli hiyo inasaidia vyombo vya habari na jopo la washauri bingwa la Kenya katika kufahamu kwa kina moyo wa Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China.