Makamu mwenyekiti wa chama tawala cha Tanzania ajiuzulu
2024-07-30 08:55:16| CRI

Chama tawala cha Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Bw. Abdulrahman Kinana amejiuzulu.

Taarifa iliyotolewa na chama hicho imesema mwenyekiti wa CCM, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi hilo lake. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, rais Hassan amesema alipenda Bw. Kinana aendelee na wadhifa huo, lakini ametoa ombi lake la kujiuzulu tangu muda mrefu uliopita akitaka kupata nafasi ya kupumzika. Rais Hassan ameongeza kuwa chama hicho kitaendelea kukuza uzoefu ulioonyeshwa na Bw. Kinana wakati alipokuwa madarakani.

Bw. Abdulrahman Kinana aliteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM mwezi Aprili mwaka 2022 akichukua nafasi ya Bw. Philip Mangula.