Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kufanya ulinzi wa mpaka, pwani na anga wa nchi kuwa wa kisasa ili kufanya uwe imara na thabiti, wakati alipokuwa akiongoza kikao cha mafunzo ya uongozi kabla ya Siku ya Jeshi ambayo itaadhimishwa Agosti 1.
Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, alisema hayo kwenye kikao cha mafunzo cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Jumanne.