Shirika la Ndege la Ethiopia linafanya kazi ili kuimarisha miundombinu na uwezo wake kupitia kujenga makao makuu mapya kwa kushirikiana na makampuni ya ujenzi ya China.
Mradi huu ulioko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, umepangwa kukamilika mwezi Agosti mwaka 2026, na unatarajiwa kuimarisha hadhi na uwezo wa shirika hilo katika sekta ya usafiri wa anga.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo sita makuu katika hatua ya kwanza, yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 67.8.
Mkurugenzi wa mkandarasi wa mradi huo, kampuni ya ujenzi na uhandisi ya China (CCECC), Bw. Wang Peng amesema ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Desemba mwaka jana, na kwamba hadi sasa umetoa nafasi 500 za ajira kwa wenyeji.