Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka huu kufanya Septemba 4 hadi 6 mjini Beijing
2024-07-31 08:53:38| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) utafanyika mjini Beijing kuanzia Septemba 4 hadi 6.

Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu itakuwa "Kuungana mikono Kuendeleza mambo ya kisasa na Kujenga Jumuiya ya Juu ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja". Wawakilishi wa mashirika husika ya kikanda ya Afrika na mashirika ya kimataifa watahudhuria mkutano huo.

Kwenye mkutano na wanahabari msemaji mwingine Lin Jian alisema mkutano wa FOCAC mwaka huu utakuwa wa nne wa wakuu wa nchi, ambapo pande hizo mbili kwa pamoja zitaendeleza urafiki, kujadili ushirikiano na kupanga siku zijazo.