Idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa kwenye jimbo la Kerala kusini mwa India jana iliongezeka hadi 66, na idadi ya majeruhi iliongezeka hadi 70.
Maporomoko makubwa matatu ya udongo yalikumba eneo la Meppadi katika wilaya ya Wayanad ya Kerala saa 8 alfajiri kwa saa za huko wakati watu wakiwa wamelala.
Kazi za uokoaji bado zinaendelea huku kukiwa na mvua kubwa. Jeshi la India limetuma wafanyakazi 225, pamoja na timu za matibabu, katika maeneo yaliyoathiriwa. Helikopta mbili za jeshi la anga la India zimeshiriki kwenye operesheni ya uokoaji.