Kenya Jumanne ilitoa wito wa kupitia tena sera ya mambo ya nje ya nchi hiyo ili kuendelea kuwa muhimu na na ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.
Waziri mkuu wa Kenya ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na diaspora Musalia Mudavadi alisema, mwelekeo wa dunia unaathiri na kufafanua upya sera ya mambo ya nje ya Kenya, hivyo mwelekeo huo lazima ufikiriwe kwenye waraka wa Sera ya mambo ya nje ya Kenya ya 2024.
Aliongeza kuwa ni lazima kuendelea kutathmini na kurekebisha sera ya mambo ya nje, ili kuhakikisha inaendelea kuwa muhimu na kuwa na ufanisi katika kuhimiza maslahi na maadili ya kitaifa.