Tume ya uchaguzi ya Uganda yatangaza tarehe ya uchaguzi wa ubunge na urais wa mwaka 2026
2024-08-01 10:25:08| cri

Tume ya uchaguzi ya Uganda (EC) imetoa mwongozo wa uchaguzi uliorekebishwa na kutangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge na rais wa mwaka 2026

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama amesema kuwa uteuzi wa wabunge na rais utafanyika tarehe 17 mwezi Septemba hadi terehe 3 mwezi Oktoba mwaka 2025. Ameongeza kuwa kampeni zitaanza wiki ya pili ya mwezi Oktoba mwakani, na zoezi la kupiga kura itafanyika tarehe 12 Januari mwaka 2026.