Tuzo za Kimataifa zinazojulikana kama Hap Awards zinatarajia kufanyika nchini Tanzania katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Agosti 10, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema kuwa tuzo hizi zimegawanywa kwenye vipengele vikuu vitatu vikiwemo vya Muziki, Mitindo na Filamu. Amefafanua kuwa kipengele cha muziki watashindanishwa wasanii wa muziki wa Dansi, Singeli Taarabu pamoja na ngoma za asili.
Aliongezea kuwa majaji watakuwepo kutoka nchini Marekani na wengine kutoka Tanzania ambao watakuwa wakifanya mchujo katika vipengele hivyo hadi kupata mshindi, kutakuwa na Vipengele vya Muziki 11, 21 Fashioni pamoja na vipengele 11 vya Filamu.