Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) tarehe 26 Julai ilifanya mkutano wa kusikiliza maoni na mapendekezo kutoka kwa viongozi wa kamati kuu za vyama vya kisiasa visivyo vya CPC, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) na wawakilishi wa watu wasio na chama juu ya hali ya sasa ya kiuchumi ya China na kazi ya uchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu.
Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping aliendesha mkutano na kutoa hotuba muhimu. Xi alisisitiza kuwa ili kufanya vizuri kazi ya uchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu, ni muhimu kutekeleza kikamilifu kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na mkutano wa pili na wa tatu wa wajumbe wote wa awamu ya 20 ya Kamati Kuu ya CPC, kushikilia kanuni kuu ya kutafuta maendeleo huku ukidumishwa utulivu, kutekeleza kikamilifu wazo jipya kuhusu kazi za kujiendeleza kwa sahihi na kwa pande zote, kuharakisha kujenga muundo mpya wa maendeleo, kuendeleza nguvu kazi mpya yenye sifa bora inayoendana na hali halisi, na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora.
Inapaswa kuimarisha zaidi mageuzi ya pande zote kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya kisasa yenye umaalumu wa China, na kutimiza malengo ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka huu bila kuyumbayumba.