Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) limeitaka Kenya kuongeza vituo vya kunyonyesha watoto nchini kote.
Mtaalamu wa lishe wa UNICEF nchini Kenya Laura Kiige amesema kuwa akina mama wanaoishi na kufanya kazi katika maeneo hayo wana fursa ndogo ya kupata likizo ya uzazi na nafasi ya kunyonyesha watoto wao.
Amebainisha kuwa Kenya ina nafasi ya kufikia ahadi ya kimataifa inayolenga kuhakikisha kuwa watoto wananyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ili kusaidia kupunguza maambukizi kama vile kuharisha na homa ya mapafu. Ameshauri kuwa vituo vyote vya kulelea watoto katika makazi yasiyo rasmi yaliyopo vituo vya mijini vinapaswa kuwa na vifaa vya kukabiliana na ukosefu wa usawa wa unyonyeshaji na kuhimiza unyonyeshaji kama muhimu kwa afya ya mtoto.