Baraza la Hong Ting lenye kauli mbiu ya "Ushirikiano kati ya China na Afrika katika kujenga mambo ya kisasa," limefanyika mjini Nairobi likivutia makumi ya washiriki, wakiwemo watunga sera, watumishi waandamizi wa sekta ya diplomasia, wanahabari na wasomi.
Kongamano hilo lililoitishwa na Ofisi ya Nairobi ya Shirika la Habari la China Xinhua, limejadili njia za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali.
Washiriki wa baraza hilo wanaona kuwa Afrika na China zina matarajio ya pamoja ya kustawi na kuwa za kisasa kupitia kushirikiana na kufunzana.
Mtaalamu wa maswala ya ushirikiano wa kimataifa wa Kenya Bw. Cavince Adhere, amesema ushirikiano wenye manufaa kati ya China na Afrika utaunda msingi wa kukuza uchumi wa kisasa, kuleta nafasi za ajira na kueneza ustawi kwa usawa.