Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Zambia
2024-08-01 08:35:06| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Zambia Bw. Mulambo Haimbe jana Jamatano hapa Beijing.

Bw. Wang Yi amesema, China inaishukuru Zambia kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China-Moja na iko tayari kuimarisha msingi wa kuaminiana, kupanua ushirikiano, na kuendelea kuungana mkono na Zambia katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya upande mwingine.

Bw. Wang ametoa wito kwa pande mbili kufufua kwa pamoja Reli ya TAZARA, kuratibu maendeleo ya maeneo yaliyoko karibu na reli hiyo, kuisaidia Zambia kubadilisha raslimali zake kuwa msukumo wa maendeleo, na kuinua uwezo wake wa kujiendeleza na kiwango chake cha viwanda.

Kwa upande wake Bw. Haimbe amesema Zambia inapenda kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi kati yake na China, kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili.