Kwa mwaliko wa rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani, mjumbe maalumu wa rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Wang Guangqian amehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais huyu atakayeendelea na wadhifa wake.
Bw. Wang Guangqian alikutana na Rais Ghazouani na kufikisha salamu za pongezi na matumaini mema kutoka kwa rais Xi Jinping na kusema China inatilia maanani kuendeleza uhusiano na Mauritania na pia inapenda kushirikiana na nchi hiyo kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano halisi, kuzidisha mawasiliano ya kiutamaduni na kuendelea kujenga mustakbali mzuri wa uhusiano kati yao.
Naye Rais Ghazouani amemtaka Bw. Wang kufikisha salamu zake za dhati kwa rais Xi na kumshukuru kwa kutuma mjumbe maalumu kuhudhuria sherehe hiyo. Amesema Mauritania inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China katika sekta mbalimbali na kuhimiza uhusiano kati yao kufikia kiwango cha juu zaidi.