Treni za umeme za SGR za Tanzania zaanza kutoa huduma kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma
2024-08-02 08:53:00| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania jana Alhamisi alizindua rasmi huduma ya treni ya umeme ya Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

Safari za majaribio kati ya miji hiyo miwili zilianza mwezi uliopita.

Rais Samia alipanda treni hiyo na kuwasili Dodoma baada ya safari ya saa tatu na nusu. Amesema, mwendokasi mkubwa wa treni hiyo utapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri na kurahisisha usafiri wenye ufanisi wa watu na mizigo nchini Tanzania.

Rais Samia amesema Serikali imeagiza mabehewa 1,430 ya mizigo, ambayo yataimarisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi maeneo ya ndani na nchi jirani zisizo na bandari, ikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).