Idara ya Misitu, Uvuvi na Mazingira ya nchini Afrika Kusini (DFFE) imesema jana, nchi hiyo imerikodi kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ujangili wa vifaru katika miezi ya Mei na Juni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Taarifa iliyotolewa na Idara hiyo imemnukuu Waziri wa Misitu, Uvuvi na Mazingira wa nchini humo Bw. Dion George akisema, hasara ya kitaifa ya vifaru iliyoripotiwa katika Mei na Juni imekuwa 21 na 22. Amesema huenda hasara hiyo imepungua kutokana na kukatwa kwa pembe za vifaru katika Mkoa wa KwaZulu-Natal, hasa katika Hifadhi ya Hluhluwe iMfolozi, ambapo zaidi ya faru 1,000 wamekatwa pembe tangu Aprili mwaka huu.