Wanasayansi wapata maendeleo makubwa katika kudhibiti maradhi yanayoletwa na mbu
2024-08-02 10:37:43| cri

Timu moja ya utafiti imetengeneza kifaa kinachojiendesha, ambacho kinaweza kuwatenganisha mbu wa kiume na wa kike kwa ufanisi, hatua ambayo ni maendeleo makubwa katika udhibiti wa kibiolojia dhidi ya maradhi yanayoletwa na mbu.

Timu hiyo ya kimataifa inaundwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan, Chuo Kikuu cha Jinan, na kampuni ya teknolojia ya kibiolojia ya Wolbaki ya Guangzhou, ambao walitangaza matokeo yao ya utafiti Jumatano kwenye jarida la akademia ya kimataifa la “Science Robotics”.