Takriban watu 17 waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye vijiji viwili vya jimbo la Gezira katikati mwa Sudan.
Kamati ya upinzani ya Wad Madani, mji mkuu wa Gezira ilisema katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa wanamgambo wa RSF walivamia kijiji cha Al-Adnab wakiwa na misafara mikubwa ya kijeshi kwa lengo la kuwapora na kuwafanyia ukatili raia. Zaidi ya watu 10 waliuawa kutokana na shambulio hilo.
Aidha kamati hiyo ilisema kuwa raia saba ambao hawakuwa na silaha pia waliuawa katika shambulio la wanamgambo katika kijiji cha Wad Al-Asha Jumatano.