Wataalamu wakutana nchini Kenya ili kuoanisha viwango vya bidhaa barani Afrika
2024-08-02 09:18:10| CRI

Wataalamu wa Afrika wamekutana huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ili kujadili kuhusu njia za kuoanisha viwango vya bidhaa barani humo.

Mkutano mkuu wa 17 wa mfumo wa metrolojia wa Afrika na mkutano wa kiufundi ulioanza Alhamis na kuendelea kwa siku tano, umewaleta pamoja maofisa wa Umoja wa Afrika na mamlaka za viwango kutoka kote barani ili kukuza maendeleo ya kuoanisha viwango vya bidhaa.

Katibu mkuu wa wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda ya Kenya Bw. Juma Mukhwana amesema, moja kati ya vyanzo vya biashara barani Afrika kuwa ya chini ni ukosefu wa utambuzi wa viwango vya biadhaa vya serikali za nchi mbalimbali barani Afrika.

Amesema, viwango vinavyofanana vitapunguza vikwazo visivyo vya kiushuru kwa bidhaa zinazotengenezwa katika nchi moja ya Afrika na kuuzwa katika nchi nyingine. Amebainisha kuwa jumuiya za kiuchumi ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki zitaharakisha kufikiwa kwa viwango vya pamoja vya bidhaa.