Africa CDC: Visa vya homa ya mpox vyaongezeka kwa asilimia 160 barani Afrika
2024-08-02 08:52:06| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha Afrika (Africa CDC) kimedokeza kuwa, nchi 15 za Afrika zimeripoti vifo 1,451 vinavyotokana na homa ya mpox tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu hali ya maambukizi ya homa ya mpox barani Afrika iliyotolewa jumatano na kituo hicho, jumla ya visa 37,583 vya homa ya mpox na vifo 1,451 vimeripotiwa katika nchi 15 wanachama wa Umoja wa Afrika tangu mwanzoni mwa mwaka 2022 hadi Julai 28, mwaka huu, kiwango cha vifo kikiwa ni asilimia 3.9.

Takwimu za kituo hicho zinaonesha kuwa idadi ya vifo na visa vipya vya homa ya mpox iliyorekodiwa mpaka sasa mwaka huu inaashiria ongezeko la asilimia 19 na asilimia 160 mtawalia, ikilinganishwa na mwaka jana muda kama huo.