Watoto wa kike waliojifungua kuruhusiwa kuendelea na masomo
2024-08-03 09:00:08| CRI

Mara nyingi kumekuwa na taarifa za watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi kukatisha masomo yao kutokana na ujauzito, jambo ambalo linabadili kabisa mwelekeo ama mipango ya maisha yao ya baadaye. Kwani mara binti anapopata ujauzito akiwa shuleni, inakuwa vigumu sana kwake kuendelea na masomo kutokana na kutengwa na wanafunzi wenzake kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni ‘tabia mbaya.’ Lakini unaweza kukuta baadhi ya mabinti hawa wanapata ujauzito kutokana na kubakwa ama kulazimishwa kufanya ngono na ndugu wa karibu, hivyo si makosa yao.

Ni kutokana na hali hiyo, wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali walianza juhudi za kupendekeza watoto wa kike waliopata ujauzito kuendelea na masomo, na wale waliojifungua kurudi tena shuleni. Wazo hili ni zuri kwa kuwa linamwezesha mtoto wa kike kupata haki yake ya elimu, lakini pia linaleta wasiwasi kuwa, baadhi ya mabinti wanaweza kupata ujauzito kwa makusudi wakiwa shuleni wakiamini kuwa, wanaweza kuendelea na masomo na pia kurejea shule wanapojifungua. Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake leo hii, tutaangazia jambo hili kwa undani zaidi.