Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Sudan wamakabiliwa na njaa kali, ikiwemo watu 755,000 wanaokabiliwa na mazingira magumu, huku vifo vinavyohusiana na njaa pia vikirekodiwa.
Dujarric amesema, maeneo 14 nchini Sudan yametangazwa kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa katika miezi ijayo.
Ameongeza kuwa, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) linaongeza kasi ya mwitikio wa dharura ili kuokoa maisha zaidi ya watu nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuongeza misaada na kutambua njia za uvumbuzi na ufanisi za kufikisha msaada wa dharura kwa mamilioni ya watu nchini Sudan, hususan katika maeneo ambayo ni magumu kufikika.