Rais Xi Jinping wa China alisema China inatakiwa kutekeleza sera ya kustawisha vijiji na kutatua pengo la maendeleo kati ya miji na vijiji ili kutimiza maendeleo ya kisasa ya China.
Mwaka huu rais Xi aliweka mpango wa maendeleo yenye uwiano kwenye mpango wa jumla wa maendeleo ya kisasa ya China, kutkeleza kwa kina mkakati wa kuhimiza maendeleo yenye uwiano ya kikanda, kuharakisha maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji na kutia nguvu maendeleo ya kisasa ya China.
Kutimiza maendeleo yenye uwiano kunalenga kutatua pengo la maendeleo ya kikanda, na kutimiza utajiri wa watu wote.