Rais Xi Jinping atoa maagizo muhimu kuhusu kuimarisha kazi ya kuhifadhi, kuenzi na kutumia urithi wa kiutamaduni na wa asili
2024-08-06 15:36:55| cri

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni ametoa maagizo muhimu kuhusu kuimarisha kazi ya kuhifadhi, kuenzi na kutumia urithi wa kitamaduni na wa asili, akisema kuorodheshwa kwa “Mhimili wa Kati wa Beijing”, “Eneo la Jangwa la Badain Jaran-Milima ya Mchanga na Maziwa”, na “Makazi ya Ndege wanaohama katika Bahari ya Njano (Bohai) ya China (Hatua ya II)” kuwa Urithi wa Dunia, kuna umuhimu mkubwa katika ujenzi wa China ya kisasa yenye uwiano kati ya ustaarabu wa kimali na wa kiroho na mapatano kati ya binadamu na maumbile, na kumeng’arisha bustani ya staarabu za dunia.

Rais Xi amesisitiza kutumia fursa ya mafanikio haya, kuimarisha zaidi uhifadhi wa urithi wa kiutamaduni na wa asili, na kuinua kihalisi kiwango na uwezo wa kuhifadhi urithi.