Wizara ya Wanawake na Mambo ya Kijamii ya Ethiopia imesaini makubaliano na Mfuko wa China kwa Maendeleo ya Vijijini (CFRD), ili kutekeleza mradi wa pamoja unaolenga kuboresha maisha ya watu maskini na jamii zilizoko katika mazingira magumu kwenye maeneo mbalimbali nchini Ethiopia.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa Jumatatu mjini Addis Ababa, yanaashiria ushirikiano wao na dhamira ya kuleta athari chanya kwa maisha ya watu wenye uhitaji.
Waziri wa Wanawake na Mambo ya Kijamii wa Ethiopia Ergogie Tesfaye alisema mfuko wa CFRD unatoa mfano mzuri katika kutoa huduma za kibinadamu nchini Ethiopia hasa katika sehemu za vijijini. Amethibitisha kuwa wizara yake inadhamiria kushirikiana na CFRD katika kutekeleza mradi huo.
Mkurugenzi wa CFRD kwenye ofisi ya Ethiopia Yin Qian alisema mradi huo utatekelezwa mara moja baada ya makubaliano kusainiwa.