China yaitaka ICC kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama ya Sudan na maswala halali
2024-08-06 08:54:06| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Dai Bing, Jumatatu alitoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama ya Sudan na maswala halali wakati wakishughulikia kesi ya Darfur.

Bw. Dai alitoa wito huo katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ICC Sudan. Amesema China imekuwa ikifuatilia kwa karibu uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuhusu hali ya Darfur, na kwamba inakaribisha rejea ya mwendesha mashtaka katika ripoti yake ya ushirikiano wa serikali ya Sudan na mwendesha mashtaka kuhusu kesi ya Darfur, kutoa viza kwa timu ya mashtaka, na kujibu maombi kadhaa ya usaidizi.

Dai alisisitiza kuwa China siku zote inatetea suluhu ya kisiasa, ambayo ni "njia pekee inayowezekana ya kumaliza mzozo na kurejesha amani," akibainisha kuwa mazungumzo ya hivi karibuni ya huko Geneva kati ya pande hizo mbili kuhusu mzozo na mpango wa kurudisha wapatanishi Djibouti, yameunda kasi nzuri kwa upatanishi wa kimataifa na diplomasia.