Bei ya reja reja ya petrol na dizeli nchini Tanzania kwa mwezi huu wa Agosti imepanda katika mikoa inayochukua mafuta hayo kwenye bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ikilinganishwa na mwezi Julai.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini humo (EWURA) imesema, bei ya mafuta kuanzia leo jumatano imeongezeka kwa shilingi 21 kwa lita na kufikia sh 3,231 kwa mafuta yanayochukuliwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Pia kwa mafuta yanayochukuliwa katika bandari ya Tanga, bei kwa lita moja imeongezeka na kufikia sh 3,229 kutoka sh 3,210, na katika bandari ya Mtwara imefikia sh 3,304 kutoka sh 3,212.