Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus Jumatano alisema, WHO inaitisha kamati ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na kuenea kwa mpox nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na uwezekano wa kuenea zaidi duniani.
Akiongea na wanahabari mjini Geneva Tedros alisema, kamati hiyo itakutana “haraka iwezekanavyo” ili kutathmini kama mlipuko wa maradhi hayo utakuwa tukio la dharura la afya ya umma linalofuatiliwa kote duniani.