Rais wa Tunisia amfuta kazi Waziri Mkuu wake
2024-08-08 14:07:25| cri

Rais wa Tunisia Kais Saied amemfukuza kazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ahmed Hachani jana jumatano.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais imesema, rais Saied amemteua Waziri wa Masuala ya Kijamii nchini humo Kamel Maddouri kuwa Waziri Mkuu mpya, bila ya kueleza sababu za kufutwa kazi kwa waziri mkuu wa zamani.

Hachani aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tunisia mwezi Agosti mwaka jana.