Wataalamu wa upelelezi wakutana Angola kujadili usalama nchini DRC
2024-08-08 14:06:28| cri

Wataalamu wa upelelezi kutoka Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Angola wamekutana jana jumatano mjini Luanda, mji mkuu wa Angola, kujadili hali ya usalama nchini DRC.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola imesema, mkutano huo unafuatia mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo tatu uliofanyika Julai 30, ambao uliamuru kusitishwa kwa mapigano katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ambako jeshi la DRC linapambana na waasi wa kundi la M23.

Wataalamu hao wanatarajiwa kuwasilisha ripoti yao itakapofika Agosti 15, kabla ya mkutano wa tatu wa ngazi ya mawaziri, ambao pia utafanyika baadaye mwezi huu.