Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi jana alihudhuria halfa ya kusaini makubaliano ya miradi inayowekezwa na kujengwa na kampuni za China, ukiwemo mradi wa kituo cha umeme wa Photovoltaic.
Akihojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), Dk. Mwinyi amesema Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ni jukwaa muhimu la ushirikiano linalokusanya maoni ya pamoja ya maendeleo, na amesema ana matarajio makubwa na mkutano ujao wa Baraza hilo wa mwaka huu, na kwamba atajifunza uzoefu wa China wa kutokomeza umaskini ili kunufaisha watu wa huko.
Dk. Mwinyi amesisitiza kuwa, China imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, na maendeleo ya Afrika hayawezi kuondokana na China.