Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq amesema, zaidi ya nusu ya mazao nchini Zimbabwe imeharibika kutokana na ukame wa kihistoria, na kusababisha watu milioni 7.6 nchini humo kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa kali.
Amesema Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja huo imeripoti kuwa, hali ya usalama wa chakula nchini Zimbabwe inaendelea kuwa mbaya kutokana na ukame uliosababishwa na hali ya hewa ya El Nino.
Ameongeza kuwa, ukame huo umeleta shinikizo kwa uchumi wa Zimbabwe, huku zaidi ya moja ya tano ya watoto wanaotakiwa kwenda shule wakiacha shule, na pia kusababisha uhaba mkubwa wa maji.