Hojaji iliyofanywa na Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha China CGTN kuhusu tuhuma za Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli la Marekani (USADA) imeonyesha kuwa, asilimia 95.57 ya washiriki wanaamini kuwa huenda USADA inaficha ukweli kuhusu wanariadha wa Marekani wanaotumia dawa za kuongeza nguvu.
Hivi karibuni, mwanariadha kutoka nchini Marekani Erriyon Knighton alikumbwa na kashfa ya kutumia dawa za kusisimua misuli, kashfa ambayo inaleta wasiwasi kuhusiana na uaminifu wa Shirika hilo.
Katika hojaji hiyo, asilimia 90.15 ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaamini kuwa, Marekani kuficha ukweli na Knighton kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Paris kumeondoa usawa na uhalali wa mashindano hayo, huku asilimia 96.54 wakisema kuwa hatua hiyo ni mfano halisi wa vigezo viwili vinavyotumiwa na Marekani. Asilimia 95.63 wanashuku kuwa wanariadha kutoka Marekani wanahusika sana katika kutoa ripoti zisizo na ukweli.