Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda Victoria Rusoke Businge amepongeza mchango wa serikali ya China na shirika lisilo la kiserikali la China katika kulinda mazingira na kurejesha misitu nchini Uganda.
Businge alisema hayo Jumatano mjini Kampala, wakati akilikabidhi Shirika la Mamlaka ya Kanda ya Ziwa Victoria (LVRLAC) miti na miche ya matunda elfu kumi iliyochangiwa na NGO ya Mfuko wa Kuokoa Wanyama na Mimea (SWF). Pia alisisitiza ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali za miji, ikiwa ni pamoja na mji wa Entebbe nchini Uganda, na mji wa Wuhan nchini China kwenye sekta za ujenzi wa miundombinu na uungaji mkono wa mazingira.
Kansela wa uchumi na biashara wa China nchini Uganda Wang Jianxun alisema China imeanza safari mpya ya kujenga nchi ya ujamaa ya kisasa, ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira, na kuhamasisha kampuni nyingi zaidi za China zishiriki kwenye programu za uhifadhi wa mazingira na majukumu ya kijamii.