Barabara ya Dongo Kundu kukuza biashara ya kuvuka mpaka kati ya Kenya naTanzania
2024-08-12 22:59:42| cri

Biashara za kuvuka mpaka kati ya Kenya na Tanzania katika Kituo cha Mpakani cha Lunga-Lunga zitaongezeka, baada ya kukamilika kwa barabara ya Dongo Kundu itakayounganishwa na bandari ya Mombasa.

Kukamilika na kufunguliwa kwa barabara hiyo wiki hii iliyogharimu dola 307,106, ndani ya mtandao wa barabara ya bandari ya Mombasa, kutawezesha usafirishaji wa bidhaa hadi kwenye mpaka wa pili kwa shughuli nyingi zaidi kati ya Kenya na Tanzania baada ya Namanga, bila kutumia kivuko cha Likoni.

Mradi huo baadaye utaunganishwa na mradi wa maendeleo wa Njia ya Pwani ya Afrika Mashariki yenye urefu wa kilomita 460 kati ya Malindi na Bagamoyo, unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na ruzuku kutoka Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka nchi hizo mbili za biashara katika mpaka huo, Tanzania inasafirisha zaidi mazao ya kilimo kupitia mpaka huo ambapo Kenya inasafirisha bidhaa za viwandani na malighafi.