Rais Paul Kagame ambaye alichaguliwa tena kuwa rais wa Rwanda, ameapishwa jana katika Uwanja wa Amani wa Kitaifa ulioko katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali.
Katika hotuba yake, rais Kagame amesema atachukua muhula wake mpya kama mwanzo wa kazi ngumu zaidi, na lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi maisha salama, yenye afya na heshima.
Viongozi wa nchi na serikali kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika ya Kati, Msumbiji, na Kenya, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa na kikanda, na maofisa waandamizi wa serikali walihudhuria sherehe hiyo.
Rais Kagame alishinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika Julai 15, kwa kupata kura zaidi ya milioni 8.8, sawa na asilimia 99.18, na kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.