Rwanda yazipita Kenya na Tanzania katika Mbio za Unafuu wa Mtandao wa Internet
2024-08-12 11:01:05| cri

Kupaa kwa Rwanda na kuwa mbele katika kutoa huduma ya mtandao wa intaneti kwa bei nafuu kumekuwa kukivutiliwa zaidi, haswa kwa kuwa imeipita majirani zake, Kenya na Tanzania.

Takwimu kutoka kampuni ya utafiti ya teknolojia ya Uingereza Cable inatoa ushahidi wa kutosha wa maendeleo ya Rwanda. Wastani wa gharama ya mtandao wa Internet nchini Rwanda imepungua kutoka dola 60.96 hadi dola 43.22 kwa mwezi. Kupungua huku kwa asilimia 29.1 sio tu inaifanya Rwanda kuwa mfano wa azma yake ya kuimarisha upatikanaji wa intaneti bali pia kunaonesha mwelekeo mpana wa kupungua kwa gharama katika maeneo yanayoendelea.

NayoTanzania, ambayo hapo awali iliongoza chati ya uwezo wa kumudu, inaoneka kuwa na ongezeko kidogo la wastani wa gharama, ambayo sasa inafikia dola 43.44 kwa mwezi. Wakati huo huo, bei ya mtandao wa intaneti nchini Kenya ilishuka kidogo kutoka dola 49.13 hadi $47.73. Mabadiliko haya yanaonesha mazingira ya ushindani ambapo bei za watumiaji huathiriwa moja kwa moja na mienendo ya soko na ushindani baina ya nchi.