Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Iran wazungumza kwa njia ya simu
2024-08-12 08:38:43| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amezungumza kwa simu na kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Bagheri Kani jana Jumapili.

Katika mazungumzo hayo Bw. Wang amesema China inaikaribisha Iran katika shughuli zilizoandaliwa nayo ikiwa mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO). Pia amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano na Iran chini ya mfumo wa BRICS na kukuza maendeleo ya utawala wa kimataifa kwa kufuata mwelekeo wa haki na busara.

Kwa upande wake Bw. Bugheri amesisitiza kuwa rais wa Iran Masoud Pezeshkian amejikita kithabiti katika kuendeleza uhusiano kati ya nchi hiyo na China, na kuhakikisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili hautaathiriwa na mabadiliko ya hali ya kimataifa na kikanda.