Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza kuboresha uwakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama
2024-08-13 08:45:55| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuimarisha ufanisi wa uwakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja huo ili kuhakikisha uhalali na uaminifu wa Baraza hilo.

Akizungumza katika mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana kuhusu “Kukabiliana na Historia ya Kukosa Usawa na Kuimarisha Ufanisi wa Uwakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” Guterres ameema Baraza hilo limekuwa msingi wa amani na usalama wa dunia tangu mwaka 1945, lakini nyufa zilizoko katika msingi wake zinaendelea kuwa kubwa na haziwezi kupuuzwa tena.

Amesema dunia imebadilika, lakini muundo wa Baraza hilo haujakwenda na wakati, na kuongeza kuwa, haikubaliki kuwa taasisi ya amani na usalama duniani inakosa sauti ya kudumu kwa bara lenye watu zaidi ya bilioni moja, ambao wanachukua asilimia 28 ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.