China yafuatilia idadi kubwa ya vifo vya raia vilivyosababishwa na operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza
2024-08-13 08:44:08| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China ina wasiwasi mkubwa juu ya idadi kubwa ya raia waliouawa kutokana na operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza.

Li Jin amesema hayo alipozungumzia shambulio la Jeshi la anga la Israel dhidi ya shule moja katika Ukanda wa Gaza lililotokea jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.

Bw. Lin amesema China inalaani kitendo chochote kinachowaathiri raia, inapinga ukiukaji wowote wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na kuitaka Israel kusikiliza kwa makini wito wa jumuiya ya kimataifa, kusitisha mara moja mapigano na kulinda raia kwa nguvu zote, ili kuzuia hali ya wasiwasi katika kanda hiyo isizidi kuongezeke. Pia amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya juhudi za pamoja ili kupunguza na kumaliza janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.