Teknolojia ya Juncao, ambayo ni teknolojia ya upandaji wa uyoga ya China imetajwa kuhimiza uzalishaji wa kilimo cha uyoga nchini Rwanda.
Baadhi ya wakulima nchini Rwanda waliokuwa wanafunzi kama Obed Nyambo walijiajiri na kuwa wakulima wa Uyoga. Bwana Nyambo ambaye mwanzoni alikuwa mfugaji, baada ya kugundua Teknolojia ya Juncao, amejikita kwenye kilimo cha uyoga na kupata faida.
Teknolojia ya kilimo cha Uyoga ya Juncao iliyovumbuliwa kwenye miaka ya 1980 na Kituo cha Utafiti wa Uhandisi wa Kitaifa cha Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian, inawawezesha wakulima wadogo kupanda uyoga kutoka kwa nyasi kavu, zilizokatwa, bila kukata miti na kuharibu mazingira.