Ofisi ya msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 12 Agosti ilitoa taarifa ikisema, baada ya kushuhudia vifo vya watu wengi wa Gaza kutokana na shambulizi la jeshi la Israel dhidi ya shule ya Gaza, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amelaani tishio la kudumu kwa usalama wa maisha ya watu wa Gaza linaloletwa na duru hii ya mapambano kati ya Palestina na Israel.
Taarifa imesema Bw. Guterres amesikitisha kwa kutotekelezwa kwa azimio namba 2735 la Baraza la Usalama la UM, na amehimiza pande mbili zinazopambana zishiriki tena kwenye mazungumzo na kufikia makubaliano kuhusu kusitisha vita na kuwaachia huru watu wanaoshikiliwa. Amesisitiza kuwa pande zote lazima zishikilie siku zote kanuni za sheria ya kibinadamu ya kimataifa.