Kampuni ya China yawekeza katika ujenzi wa kituo kikubwa zaidi cha umeme cha nguvu ya Photovoltaic nchini Botswana
2024-08-14 08:34:20| CRI

Kampuni ya Umeme ya Botswana imesaini mkataba wa ununuzi wa umeme na Kampuni ya Sinotswana Green Energy, na kuanza rasmi ujenzi wa kituo cha kwanza cha umeme wa nguvu ya Photovoltaic cha megawati 100 nchini Botswana.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi amesema huu ni mradi muhimu wa Botswana unaoendana na malengo ya sera za nishati ya nchi hiyo ambayo yanaweza kuzalisha nishati inayoweza kumudu, ya kuaminika na ya kutosha kwa maendeleo endelevu.

Balozi mdogo wa mambo ya uchumi katika Ubalozi wa China nchini Botswana Lan yuqiang amesema, China iko tayari kubadilishana uzoefu wa kuendeleza nishati ya kijani na Botswana, na kuhamasisha makampuni mengi zaidi ya China kuwekeza katika sekta ya nishati mpya nchini Botswana.