Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Bw. Thomas Bach amemtumia barua mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong, akipongeza mafanikio makubwa ya CMG katika kutangaza Michezo ya Olimpiki ya Paris, pia aliwashukuru wafanyakazi wote wa CMG walioshiriki kwenye utangazaji huo.
Amesema, michezo hiyo isingepata mafanikio makubwa kama hayo bila ya uungaji mkono na juhudi za CMG.
Kwenye barua yake, Bw. Bach amesema Michezo ya Olimpiki ya Paris ya mwaka 2024 imemalizika kwa mafanikio, na CMG imefanya kazi muhimu kwenye kipindi cha michezo hiyo.