Mlipuko wa kipindupindu wasababisha vifo vya watu 17 nchini Sudan
2024-08-14 23:05:21| cri

Wizara ya Afya ya Sudan imesema, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umetokea katika wilaya saba za majimbo matatu nchini humo, ambapo kesi 268 za ugonjwa huo zimeripotiwa pamoja na vifo 17. Licha ya hayo, maambukizi ya ugonjwa wa macho pia yameenea katika majimbo tisa ya nchi hiyo, huku kesi 2,689 zikiripotiwa na wengi kati yao ni waliopoteza makazi. Wizara hiyo imetenga fedha za dharura kuimarisha udhibiti na kinga ya magonjwa hayo.