Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) jana kimetangaza ugonjwa wa Mpox kuwa janga la afya ya umma barani humo, na kuzitaka nchi za Afrika kuchukua hatua za haraka ili kuzuia ugonjwa huo kuendelea kuenea katika bara hilo.
Mkurugenzi wa Africa CDC Bw. Jean Kaseya amesema, uamuzi huo utasaidia kukusanya rasilimali kwa kiasi kikubwa, kuimarisha utaratibu wa kimataifa wa kutoa taarifa, na kukabiliana vyema na janga hilo.
Takwimu kutoka Kituo hicho za Alhamis iliyopita zilionyesha kuwa nchi 16 barani Afrika zimeathiriwa na ugonjwa wa Mpox.
Afrika imeripoti ongezeko la asilimia 160 la maambukizi ya Mpox mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka jana.