Serikali ya mpito ya Afghanistan yasema mapambano yametokea kati ya jeshi lake na jeshi la Pakistan katika eneo la mpakani
2024-08-14 10:04:58| cri

Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya mpito ya Afghanistan imesema mapambano yalitokea kati ya jeshi lake na jeshi la Pakistan usiku wa tarehe 12 mwezi huu katika kivuko cha Torkham mpakani na kusababisha vifo vya raia watatu wa Afghanistan. Kwa mujibu afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, wanajeshi watatu wa Pakistan walijeruhiwa katika mapambano hayo.

Jeshi la Pakistan halijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.