Wakulima wa Tanzania watakuwa kuchangamkia soko la mashudu ya Alizeti nchini China
2024-08-15 23:00:36| cri

Wakulima wa alizeti pamoja na mazao mengine yakiwemo tumbaku, pilipili na parachichi wamehakikishiwa uwepo wa masoko ya mazao yao nchini China, huku Serikali ikiendelea na juhudi za kufufua masoko katika nchi nyingine Duniani.

Naibu Waziri wa Kilimo wa Tanzania Bw. David Silinde na Ofisa wa Mamlaka ya Forodha ya China, Bw. Yu Jianhua wamesema hayo baada ya kusaini kumbukumbu ya maelewano kuhusu biashara ya mashudu ya alizeti nchini China, iliyosainiwa na katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje mjini Dar es Salaam.

Bw. Silinde amesema wamepata fursa hiyo baada ya mazungumzo, na mbali na hilo China imekubali makampuni takribani tisa kutoka Tanzania yanayoruhusiwa kusafirisha zao la parachichi, bila kumlazimu mkulima au mfanyabiashara kusafirisha kupitia nchi jirani kama ilivyokuwa hapo awali.

Bw. Silinde pia amesema Bw. Yu Jianhua amemthibitishia kwamba watatuma timu ya wataalam kuharakisha utekelezaji wa sehemu za makubaliano ikiwemo upelekaji wa pilipili nchini China, usafirishaji wa zao la tumbaku.