Msemaji wa jeshi la polisi mjini Kampala, Uganda, Patrick Onyango jana amesema, idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya maporomoko ya dampo la Kawempe katika mji huo imefikia 30.
Msemaji huyo amesema, miili 6 ya watu wenye umri wa kati ya miaka mitatu na 33 iligunduliwa kwenye dampo hilo.
Kutokana na uchunguzi wa kamati ya usajili, takriban watu 39 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi katika vijiji vitatu vilivyoathirika vya Lusanja, Kitetika na Kiteezi.