Rais wa China atoa wito kwa watu wanaojitolea kuhifadhi mazingira kuhimiza uhifadhi wa maji
2024-08-15 14:58:38| cri

Rais Xi Jinping wa China amewatia moyo wafanyakazi wa kujitolea wa kuhifadhi mazingira kuhimiza uhifadhi wa maji na kutoa mchango kuleta mambo ya kisasa kwenye mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili.

Kabla ya siku ya pili ya kimataifa ya ikolojia ya China inayoangukia Alhamisi, rais Xi amesema kwenye barua kwa watu wanaojitolea kwenye hifadhi ya Danjiangkou mjini Shiyan, mkoani Hubei, katikati ya China.

Danjiangkou ni chanzo cha maji cha njia ya kati ya mradi wa kusafirisha maji kutoka kusini hadi kaskazini. Rais Xi alitoa maagizo muhimu wakati awamu ya kwanza ya njia hiyo ilipoanza kutoa maji mwaka 2014.

Katika muongo uliopita, juhudi nyingi zimefanywa katika ulinzi wa ubora wa maji ya bwawa, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa maofisa na wakazi wa huko wakiwemo watu wanaojitolea wa kulinda mazingira. Hivi karibuni, wafanyakazi hao walimwandikia barua rais Xi kuripoti huduma zao na kueleza dhamira yao thabiti ya kulinda ubora wa maji katika bwawa.